Pular para o conteúdo
Publicidade

Mal

Por Bíblia Online

A existência do mal é realidade que a Bíblia confronta diretamente. Deus não é autor do mal, mas nos dá armas para vencê-lo e promete que o bem sempre prevalecerá.

Separar-se do mal

O temor do Senhor é aborrecer o mal. A Bíblia nos exorta a odiar o pecado, guardar os pés do mal e fugir de toda aparência maligna.

Kumcha Mwenyezi Mungu ni kuchukia uovu;

ninachukia kiburi na majivuno,

tabia mbaya na mazungumzo potovu.

Wale wanaompenda Mwenyezi Mungu na wauchukie uovu,

kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake

na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.

Aache uovu, atende mema,

aitafute amani na kuifuatilia.

Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako,

usiache dhambi yoyote initawale.

"Jiosheni na mkajitakase.

Yaondoeni matendo yenu maovu mbele zangu;

acheni kutenda mabaya.

Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;

mche Mwenyezi Mungu ukajiepushe na uovu.

Hii itakuletea afya mwilini mwako,

na lishe kwenye mifupa yako.

Vencer o mal com o bem

Não te deixes vencer do mal, mas vence o mal com o bem. A luz brilha nas trevas, e as trevas não prevalecem contra ela.

Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Alama za Mfuasi wa kweli wa Al-Masihi

Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.

Maelekezo ya mwisho

Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na kujiepusha na wale watu waletao matengano na kuweka vikwazo mbele yenu dhidi ya mafundisho mliyojifunza.

Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda.

Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. Jiepusheni na uovu wa kila namna.

Proteção contra o mal

Deus nos livra do mal e guarda nossos passos. Devemos nos revestir da armadura de Deus para resistir às forças das trevas.

Usitutie majaribuni,

bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu

[kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu,

na utukufu, hata milele. Amen].

Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu.

Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.

Bwana Isa ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe milele na milele. Amen.

Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kuzipinga hila za ibilisi.

Kwa maana kushindana kwetu si dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya falme na mamlaka, dhidi ya wakuu wa ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, wala msimpe ibilisi nafasi.

Deus transforma o mal em bem

O que o mal pretendeu contra nós, Deus transformou em bem. Ele tira pureza da aflição e confessa a restauração dos arrependidos.

Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi.

Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu.

Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutokana na udhalimu wote.

Akaendelea kusema, "Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi."

Chuki huchochea faraka,

lakini upendo husitiri mabaya yote.

"Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Fanyeni hukumu za haki, onesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. Msimdhulumu mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.

Seja o primeiro

Este artigo te tocou? Faça uma oração!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.