Marido e mulher
O casamento é aliança sagrada entre marido e mulher, instituída por Deus desde o Éden. A Bíblia define papéis complementares fundados em amor, respeito e fidelidade mútua.
Instituição divina
Deus criou homem e mulher e os uniu em uma só carne. O casamento é projeto divino que reflete o amor de Cristo pela Igreja.
Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,
kwa mfano wa Mungu alimuumba;
mwanaume na mwanamke aliwaumba.
Bwana Mwenyezi Mungu akasema, "Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa."
Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Akawajibu, "Je, hamkusoma kwamba hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe."
Je, Mwenyezi Mungu hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake.
Papéis no casamento
O marido ama e a mulher respeita. Ambos se submetem voluntariamente a Deus e um ao outro, em parceria e unidade.
Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Al-Masihi alivyoipenda jumuiya ya waumini na akajitoa kwa ajili yake, kusudi aifanye takatifu, akiitakasa kwa kuiosha kwa maji katika neno lake, apate kujiletea jumuiya tukufu isiyo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na isiyo na hatia. Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Al-Masihi anavyoitunza jumuiya yake ya waumini.
Mafundisho kuhusu wake na waume
Ninyi wake, watiini waume zenu kama vile mnavyomtii Bwana Isa. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Al-Masihi alivyo kichwa cha jumuiya ya waumini, ambayo ni mwili wake, naye Al-Masihi ni Mwokozi wake. Basi, kama vile jumuiya ya waumini wanavyomtii Al-Masihi, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.
Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.
Kanuni katika madaraka ya nyumbani
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana Isa.
Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe wakali kwao.
Mafundisho kwa wake na waume
Kadhalika enyi wake, watiini waume zenu, ili kama kunao wasioamini lile neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno, kwa kuuona utakatifu na uchaji wa Mungu katika maisha yenu.
Vivyo hivyo ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa kuwajali, nanyi wapeni heshima mkitambua ya kuwa wao ni wenzi walio dhaifu, na kama warithi pamoja nanyi wa kipawa cha neema cha uzima, ili kusiwepo na chochote cha kuzuia maombi yenu.
Fidelidade e união
O casamento é honroso e deve ser preservado com fidelidade. O cordão de três dobras não se rompe facilmente.
Wawili ni afadhali kuliko mmoja,
kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:
Kama mmoja akianguka,
mwenzake atamwinua.
Lakini ni jambo la kuhuzunisha
kwa mtu yule aangukaye
naye hana wa kumwinua!
Pia, kama wawili wakilala pamoja
watapashana joto.
Lakini ni vipi mtu aweza
kujipasha joto mwenyewe?
Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa,
watu wawili wanaweza
kumkabili adui na kumshinda.
Kamba ya nyuzi tatu
haikatiki kwa urahisi.
Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata?
Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.
Mume wake anamwamini kikamilifu,
wala hakosi kitu chochote cha thamani.
Mtu anayepata mke anapata kitu chema,
naye anajipatia kibali kwa Mwenyezi Mungu.
Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi,
bali mke mwenye busara hutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Mke mwenye tabia nzuri ni taji la mumewe,
bali aaibishaye ni kama uozo
katika mifupa ya mumewe.
Chemchemi yako na ibarikiwe
na umfurahie mke wa ujana wako.
Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri:
matiti yake na yakutosheleze siku zote,
nawe utekwe daima na upendo wake.
Permanecer juntos
O que Deus uniu, o homem não separe. A Bíblia protege o casamento e orienta sobre convivência, perdão e perseverança conjugal.
Kuhusu ndoa
Basi kuhusu mambo yale mliyoyaandika: "Ni vyema mwanaume asimguse mwanamke." Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe. Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe. Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda, ili mweze kujitoa kwa maombi. Kisha mrudiane tena, ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.
Kwa wale waliooana nawapa amri (si mimi, ila ni Bwana Isa): Mke asitengane na mumewe. Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.
Lakini kama yule asiyeamini akijitenga, basi afanye hivyo. Katika hali kama hiyo mwanamke au mwanaume aaminiye hafungwi, kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani. Wewe mke, unajuaje kama utamwokoa mumeo? Au wewe mume, unajuaje kama utamwokoa mkeo?
Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka sheria ya ndoa.
Kama mtu ameoa karibuni, kamwe asipelekwe vitani au kupewa wajibu mwingine wowote. Kwa mwaka mmoja atakuwa huru kubaki nyumbani ili amfurahishe mke aliyemwoa.