Mentira
A mentira é condenada pela Bíblia como pecado grave. Deus é verdade, e quem mente se alinha com o pai da mentira. O cristão é chamado a falar a verdade em amor.
Deus odeia a mentira
Os lábios mentirosos são abominação para o Senhor. A Bíblia adverte que todo mentiroso terá parte no lago de fogo.
Mwenyezi Mungu anachukia sana midomo idanganyayo,
bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."
Kuna vitu sita anavyovichukia Mwenyezi Mungu,
naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:
macho ya kiburi,
ulimi udanganyao,
mikono imwagayo damu isiyo na hatia,
moyo uwazao mipango miovu,
miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,
shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,
na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.
Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake,
Falar a verdade
Despojai-vos da mentira e falai a verdade cada um com o próximo. Cristo é a verdade, e nos chama a ser testemunhas fiéis.
Kanuni za maisha mapya
Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.
Isa akawaambia, "Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.
Ninyi ni watoto wa baba yenu, ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli, maana hamna kweli ndani yake. Anaposema uongo, yeye husema lugha yake ya asili kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.
Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo ataangamia.
Mdanganyifu hatakaa
nyumbani mwangu,
yeye asemaye kwa uongo
hatasimama mbele yangu.
Consequências da falsidade
A mentira destrói confiança e relacionamentos. As Escrituras alertam sobre os frutos amargos do engano e da falsidade.
Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo
ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.
Midomo isemayo kweli hudumu milele,
bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.
Ulimi wa uongo huwachukia wale unaowaumiza,
nacho kinywa cha kujipendekeza husababisha uharibifu.
Unawaangamiza wasemao uongo.
Mwenyezi Mungu huwachukia
wanaomwaga damu na wadanganyifu.
" ‘Usiibe.
" ‘Usiseme uongo.
" ‘Msidanganyane.