Pular para o conteúdo
Publicidade

Pais e filhos

Por Bíblia Online

A relação entre pais e filhos é uma das mais preciosas na Bíblia. Deus estabeleceu a família como escola de fé, amor e formação de caráter.

Honrar pai e mãe

Honrar os pais é o primeiro mandamento com promessa. Os filhos são chamados a obedecer, respeitar e cuidar de seus pais.

Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

Watoto na wazazi

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.

Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.

Msikilize baba yako aliyekuzaa,

Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.

Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye,

Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama.

Amlaaniye babaye au mamaye,

Taa yake itazimika katika giza kuu.

Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.

Instruir os filhos

Os pais devem instruir os filhos no caminho certo. A educação começa cedo, com disciplina amorosa e ensino constante da Palavra.

Mlee mtoto katika njia impasayo,

Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

Maonyo juu ya kushirikiana na waovu

Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,

Wala usiiache sheria ya mama yako,

Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako,

Na mikufu shingoni mwako.

Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

Fimbo na maonyo hutia hekima;

Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.

Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe;

Bali yeye ampendaye humrudi mapema.

Ni kwa ajili ya kuonywa mnastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyeonywa na babaye?

Filhos como bênção

Os filhos são herança do Senhor. A coroa dos velhos são os filhos dos filhos, e a glória dos filhos são seus pais.

Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA,

Uzao wa tumbo ni thawabu.

Kama mishale mkononi mwa shujaa,

Ndivyo walivyo watoto wa ujanani.

Heri mtu yule

Aliyelijaza podo lake hivyo.

Naam, hawataona aibu

Wanaposema na adui langoni.

Wana wa wana ndio taji la wazee,

Na utukufu wa watoto ni baba zao.

Baba yake mwenye haki atashangilia;

Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.

Mithali za Sulemani

Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;

Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au akimwomba samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.

Seja o primeiro