Descansar no Senhor
Descansar no Senhor é um ato de fé. Em um mundo agitado, Deus nos convida a entregar nossas ansiedades, aquietar o coração e confiar plenamente em sua provisão e cuidado.
O convite ao descanso
Jesus convida os cansados e sobrecarregados a irem a Ele e encontrar descanso para as suas almas. O jugo dele é leve.
"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsi zenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi."
Tulia mbele za Mwenyezi Mungu
na umngojee kwa uvumilivu;
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,
wanapotekeleza mipango yao miovu.
"Tulieni, mjue kwamba mimi ndimi Mungu;
nitatukuzwa katikati ya mataifa,
nitatukuzwa katika dunia."
Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote,
miminieni mioyo yenu kwake,
kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.
Confiança e paz
Quem confia no Senhor encontra paz perfeita. A ansiedade perde o poder quando entregamos tudo nas mãos do Deus soberano.
Utamlinda katika amani kamilifu
yeye ambaye moyo wake ni thabiti
kwa sababu anakutumaini wewe.
Hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:
"Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,
katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,
lakini hamkutaka.
Matunda ya haki yatakuwa amani,
matokeo ya haki yatakuwa utulivu
na matumaini milele.
bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu
atafanya upya nguvu zao.
Watapaa juu kwa mabawa kama tai;
watapiga mbio wala hawatachoka,
watatembea kwa miguu wala hawatazimia.
Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Al-Masihi Isa.
Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.
Esperar no Senhor
Esperar no Senhor renova as forças. A Bíblia nos ensina que aquietar-se diante de Deus e confiar em seu tempo é marca da maturidade espiritual.
Mngojee Mwenyezi Mungu;
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
na umngojee Mwenyezi Mungu.
Nilimngoja Mwenyezi Mungu kwa saburi,
naye akanijia na kusikia kilio changu.
Mtwike Mwenyezi Mungu fadhaa zako,
naye atakutegemeza,
hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
Katika hasira yako, usitende dhambi.
Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu,
mkiichunguza mioyo yenu.
Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wale wanaomtumaini,
na kwa yule anayemtafuta;
ni vyema kungojea kwa utulivu
kwa ajili ya wokovu wa Mwenyezi Mungu.
A fidelidade de Deus
Deus é fiel. Seus planos são de paz e esperança. Podemos descansar sabendo que Ele guarda e sustenta quem nele confia.
Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wote.
"Lakini amebarikiwa mtu anayemtumaini Mwenyezi Mungu,
ambaye matumaini yake ni katika Mwenyezi Mungu.
Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji
uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji.
Hauogopi wakati wa joto ujapo;
majani yake ni mabichi daima.
Hauna hofu katika mwaka wa ukame
na hautaacha kuzaa matunda."
Mwenyezi Mungu akajibu, "Uso wangu utaenda pamoja nawe, nami nitakupa raha."
Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.
Mfalme akawaambia Yuda, "Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, tulimtafuta naye ametupatia amani kila upande." Hivyo wakajenga na wakafanikiwa.
Walipokuwa wakiteremka kuelekea mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, "Mwambie mtumishi atangulie mbele yetu." Naye mtumishi akafanya hivyo. "Subiri hapa kidogo ili nipate kukupa ujumbe kutoka kwa Mungu."