Publicidade

Salmos 121

Mwenyezi Mungu mlinzi wetu
Wimbo wa kwenda juu.

1 Nayainua macho yangu natazama milima:

msaada wangu utatoka wapi?

2 Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu,

Muumba wa mbingu na dunia.

3 Hatauacha mguu wako uteleze,

yeye akulindaye hatasinzia,

4 hakika, yeye alindaye Israeli

hatasinzia wala hatalala usingizi.

5 Mwenyezi Mungu anakulinda,

Mwenyezi Mungu ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

6 jua halitakudhuru mchana,

wala mwezi wakati wa usiku.

7 Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

8 Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-