Publicidade

Salmos 98

Mwenyezi Mungu Mtawala wa dunia
Zaburi.

1 Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya,

kwa maana ametenda mambo ya ajabu;

kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu

umemfanyia wokovu.

2 Mwenyezi Mungu ameufanya wokovu wake ujulikane

na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.

3 Ameukumbuka upendo wake

na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;

miisho yote ya dunia imeuona

wokovu wa Mungu wetu.

4 Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote,

ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

5 mwimbieni Mwenyezi Mungu kwa kinubi,

kwa kinubi na sauti za kuimba,

6 kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:

shangilieni kwa furaha mbele za Mwenyezi Mungu, aliye Mfalme.

7 Bahari na ivume na kila kilicho ndani yake,

dunia na wote wanaoishi ndani yake.

8 Mito na ipige makofi,

milima na iimbe pamoja kwa furaha,

9 vyote na viimbe mbele za Mwenyezi Mungu,

kwa maana yuaja kuhukumu dunia.

Atahukumu dunia kwa haki

na mataifa kwa haki.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-