Publicidade

Salmos 137

Maombolezo ya Israeli uhamishoni

1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza

tulipokumbuka Sayuni.

2 Kwenye miti ya huko

tulitundika vinubi vyetu,

3 kwa maana huko hao waliotuteka

walitaka tuwaimbie nyimbo;

watesi wetu walidai nyimbo za furaha;

walisema, "Tuimbieni wimbo mmoja

kati ya nyimbo za Sayuni!"

4 Tutaimbaje nyimbo za Mwenyezi Mungu,

tukiwa nchi ya kigeni?

5 Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu,

basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.

6 Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu

kama sitakukumbuka wewe,

kama nisipokufikiri Yerusalemu

kuwa furaha yangu kubwa.

7 Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, walichokifanya Waedomu,

siku ile Yerusalemu ilipoanguka.

Walisema, "Bomoa, bomoa

hata misingi yake!"

8 Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa,

heri yeye atakayekulipiza wewe

kwa yale uliyotutenda sisi:

9 yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga

na kuwaponda juu ya miamba.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-