Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 150

Msifuni Mwenyezi Mungu kwa ukuu wake

1 Msifuni Mwenyezi Mungu.150:1 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 150:6.

Msifuni Mungu katika patakatifu pake,

msifuni katika mbingu zake kuu.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu,

msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,

msifuni kwa kinubi na zeze,

4 msifuni kwa matari na kucheza,

msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

5 msifuni kwa matoazi yaliayo,

msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila chenye pumzi na kimsifu Mwenyezi Mungu.

Msifuni Mwenyezi Mungu!

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também