Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 129

Maombi dhidi ya adui za Israeli

Wimbo wa kwenda juu.

1 Wamenitesa sana tangu ujana wangu;

Israeli na aseme sasa:

2 wamenitesa sana tangu ujana wangu,

lakini bado hawajanishinda.

3 Wakulima wamelima mgongo wangu,

na kufanya mifereji yao mirefu.

4 Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki;

amenifungua toka kamba za waovu.

5 Wale wote wanaoichukia Sayuni

na warudishwe nyuma kwa aibu.

6 Wawe kama majani juu ya paa,

ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,

wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8 Wale wapitao karibu na wasiseme,

"Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako;

tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também