Publicidade

Salmos 28

Kuomba msaada
Zaburi ya Daudi.

1 Ninakuita wewe, Ee Mwenyezi Mungu, Mwamba wangu;

usikatae kunisikiliza.

Kwa sababu ukinyamaza

nitafanana na walioshuka shimoni.

2 Sikia kilio changu nikikuomba unihurumie,

ninapokuita ili unisaidie,

ninapoinua mikono yangu kuelekea

Patakatifu pa Patakatifu pako.

3 Usiniburute pamoja na waovu,

pamoja na hao watendao mabaya,

ambao huzungumza na majirani zao maneno mazuri,

lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

4 Walipe sawasawa na matendo yao,

sawasawa na matendo yao maovu;

walipe sawasawa na kazi za mikono yao,

uwalipe wanavyostahili.

5 Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Mwenyezi Mungu,

na yale ambayo mikono yake imetenda,

atawabomoa na kamwe

hatawajenga tena.

6 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu,

kwa maana amesikia kilio changu

nikimwomba anihurumie.

7 Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa.

Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

8 Mwenyezi Mungu ni nguvu ya watu wake,

ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.

9 Waokoe watu wako na uubariki urithi wako;

uwe mchungaji wao na uwabebe milele.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-