Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 70

Kuomba msaada

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.

1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;

Ee Mwenyezi Mungu, njoo hima unisaidie.

2 Wale wanaotafuta kuniua,

waaibishwe na kufadhaishwa;

wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,

warudishwe nyuma kwa aibu.

3 Wale wanaoniambia, "Aha! Aha!"

na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.

4 Lakini wote wanaokutafuta

washangilie na kukufurahia,

wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme,

"Mwenyezi Mungu ni mkuu!"

5 Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji;

Ee Mungu, unijie haraka.

Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;

Ee Mwenyezi Mungu, usikawie.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também