Publicidade

Salmos 125

Usalama wa watu wa Mwenyezi Mungu
Wimbo wa kwenda juu.

1 Wale wamtumainio Mwenyezi Mungu ni kama Mlima Sayuni,

ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.

2 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,

ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowazunguka watu wake

sasa na hata milele.

3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi

waliyopewa wenye haki,

ili wenye haki wasije wakatumia

mikono yao kutenda ubaya.

4 Ee Mwenyezi Mungu, watendee mema walio wema,

wale walio wanyofu wa moyo.

5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,

Mwenyezi Mungu atawafukuza pamoja na watenda maovu.

Amani iwe juu ya Israeli.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-18_14-04-22-