Publicidade

Salmos 14

Uovu wa wanadamu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Mpumbavu anasema moyoni mwake,

"Hakuna Mungu."

Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa;

hakuna hata mmoja atendaye mema.

2 Mwenyezi Mungu anawachungulia wanadamu

kutoka mbinguni

aone kama kuna mwenye hekima,

yeyote anayemtafuta Mungu.

3 Wote wamepotoka,

wote wameoza pamoja;

hakuna atendaye mema,

naam, hakuna hata mmoja!

4 Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza:

wale ambao huwala watu wangu

kama watu walavyo mkate,

hao ambao hawamwiti Mwenyezi Mungu?

5 Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,

maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.

6 Ninyi watenda maovu mnakwamisha mipango ya maskini,

bali Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio lao.

7 Laiti wokovu wa Israeli

ungekuja kutoka Sayuni!

Mwenyezi Mungu anaporejesha

wafungwa wa watu wake,

Yakobo na ashangilie,

Israeli na afurahi!

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-