Publicidade

Eclesiastes 4

Uonevu, taabu, uadui

1 Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua:

Nikaona machozi ya waliodhulumiwa,

wala hawana mfariji;

uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowadhulumu,

lakini hawakuwa na mfariji.

2 Nami nikasema kwamba wafu,

waliokwisha kufa,

wana furaha kuliko watu walio hai,

ambao bado wanaishi.

3 Lakini aliye bora kuliko hao wawili

ni yule ambaye hajazaliwa bado,

ambaye hajaona ule uovu

unaofanyika chini ya jua.

4 Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

5 Mpumbavu hukunja mikono yake

na kujiangamiza mwenyewe.

6 Afadhali konzi moja pamoja

na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu

na kukimbiza upepo.

7 Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua:

8 Kulikuwa na mtu aliye peke yake,

hakuwa na mwana wala ndugu.

Hapakuwa na mwisho wa kazi yake;

hata hivyo macho yake

hayakutosheka na utajiri wake.

Aliuliza, "Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani,

nami kwa nini ninajinyima kufurahia?"

Hili pia ni ubatili,

ni shughuli yenye taabu!

9 Wawili ni afadhali kuliko mmoja,

kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:

10 Kama mmoja akianguka,

mwenzake atamwinua.

Lakini ni jambo la kuhuzunisha

kwa mtu yule aangukaye

naye hana wa kumwinua!

11 Pia, kama wawili wakilala pamoja

watapashana joto.

Lakini ni vipi mtu aweza

kujipasha joto mwenyewe?

12 Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa,

watu wawili wanaweza

kumkabili adui na kumshinda.

Kamba ya nyuzi tatu

haikatiki kwa urahisi.

Maendeleo ni ubatili

13 Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo. 14 Kijana huyo angeweza kutokea gerezani akapata ufalme, au angeweza kuwa amezaliwa katika umaskini kwenye huo ufalme. 15 Nikaona kwamba wote walioishi na kutembea chini ya jua walimfuata kijana, aliyepokea ufalme. 16 Hapakuwa na kikomo cha watu wote aliowatawala. Lakini wale waliokuja baadaye hawakufurahia kazi ya yule aliyepokea ufalme. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

Veja também

Publicidade
Eclesiastes
Ver todos os capítulos de Eclesiastes
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-