Publicidade

Salmos 1

Furaha ya kweli

1 Heri mtu yule ambaye haendi

katika shauri la watu waovu,

wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,

au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

2 Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu,

naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana.

3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa

kando ya vijito vya maji,

ambao huzaa matunda kwa majira yake

na majani yake hayanyauki.

Lolote afanyalo hufanikiwa.

Huzuni ya waovu

4 Sivyo walivyo waovu!

Wao ni kama makapi

yanayopeperushwa na upepo.

5 Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,

wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

6 Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki,

bali njia za waovu zitaangamia.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-