Publicidade

Salmos 11

Kumtumaini Mwenyezi Mungu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Kwa Mwenyezi Mungu ninakimbilia.

Unawezaje basi kuniambia:

"Ruka kama ndege utorokee kwenye mlima wako.

2 Hebu tazama, waovu wanapinda nyuta zao;

wanaweka mishale kwenye nyuzi zake

ili wakiwa gizani, wawapige

walio wanyofu wa moyo.

3 Wakati misingi imeharibiwa,

mwenye haki anaweza kufanya nini?"

4 Mwenyezi Mungu yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;

Mwenyezi Mungu yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.

Huwaangalia wana wa watu,

macho yake yanawachunguza.

5 Mwenyezi Mungu huwachunguza wenye haki,

lakini nafsi yake inachukia waovu

na wale wanaopenda mapigano.

6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali

na kiberiti kinachowaka;

upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

7 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye haki,

yeye hupenda haki.

Wanyofu watauona uso wake.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-