Publicidade

Salmos 99

Mwenyezi Mungu Mfalme mtakatifu

1 Mwenyezi Mungu anatawala,

mataifa na yatetemeke;

anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,

dunia na itikisike.

2 Mwenyezi Mungu ni mkuu katika Sayuni;

ametukuzwa juu ya mataifa yote.

3 Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:

yeye ni mtakatifu!

4 Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,

wewe umethibitisha adili;

katika Yakobo umefanya

yaliyo haki na sawa.

5 Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;

yeye ni mtakatifu.

6 Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,

Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;

walimwita Mwenyezi Mungu,

naye aliwajibu.

7 Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;

walizishika sheria zake na amri alizowapa.

8 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

ndiwe uliyewajibu,

kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,

ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.

9 Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,

kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-