Publicidade

Salmos 93

Mwenyezi Mungu ni mkuu

1 Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu;

Mwenyezi Mungu amejivika utukufu

tena amejivika nguvu.

Dunia imewekwa imara,

haitaondoshwa.

2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;

wewe umekuwa tangu milele.

3 Bahari zimepaza, Ee Mwenyezi Mungu,

bahari zimepaza sauti zake;

bahari zimepaza sauti za mawimbi yake.

4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,

ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:

Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu.

5 Ee Mwenyezi Mungu, sheria zako ni imara;

utakatifu umepamba nyumba yako

pasipo mwisho.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-