Publicidade

Salmos 122

Sifa kwa Yerusalemu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,

"Twende nyumbani mwa Mwenyezi Mungu."

2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama

malangoni mwako.

3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji

ulioshikamana pamoja.

4 Huko ndiko makabila hukwea,

makabila ya Mwenyezi Mungu,

kulisifu jina la Mwenyezi Mungu kulingana na maagizo

waliopewa Israeli.

5 Huko viti vya hukumu hukaa,

viti vya ufalme vya nyumba ya Daudi.

6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:

"Wote wanaokupenda na wawe salama.

7 Amani na iwe ndani ya kuta zako,

na usalama ndani ya ngome zako."

8 Kwa ajili ya ndugu na rafiki zangu,

nitasema, "Amani iwe ndani yako."

9 Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

nitatafuta mafanikio yako.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-18_10-32-54-