Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 110

Mwenyezi Mungu na mfalme wake mteule

Zaburi ya Daudi.

1 Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu:

"Keti mkono wangu wa kuume,

hadi nitakapowafanya adui zako

kuwa mahali pa kuweka miguu yako."

2 Mwenyezi Mungu ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;

utatawala katikati ya adui zako.

3 Askari wako watajitolea kwa hiari

katika siku yako ya vita.

Ukiwa umevikwa fahari takatifu,

kutoka tumbo la mapambazuko

utapokea umande wa ujana wako110:3 au vijana wako watakujia kama umande.

4 Mwenyezi Mungu ameapa,

naye hatabadilisha mawazo yake:

"Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki."

5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,

atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga

na kuwaponda watawala wa dunia nzima.

7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia110:7 au Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka;;

kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também