Publicidade

Salmos 124

Shukrani kwa ukombozi wa Israeli
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1 Kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu;

Israeli na aseme sasa:

2 kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu,

watu walipotushambulia,

3 hasira yao ilipowaka dhidi yetu,

wangetumeza tukiwa hai,

4 mafuriko yangegharikisha,

maji mengi yangetufunika,

5 maji yaendayo kasi

yangetuchukua.

6 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu,

ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.

7 Tumeponyoka kama ndege

kutoka mtego wa mwindaji;

mtego umevunjika,

nasi tumeokoka.

8 Msaada wetu ni katika jina la Mwenyezi Mungu,

Muumba wa mbingu na dunia.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-