Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 130

Kumngojea Mwenyezi Mungu

Wimbo wa kwenda juu.

1 Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Mwenyezi Mungu.

2 Ee Bwana, sikia sauti yangu.

Masikio yako na yawe masikivu

kwa kilio changu unihurumie.

3 Kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,

Ee Bwana, ni nani angeweza kusimama?

4 Lakini kwako kuna msamaha,

kwa hiyo wewe unaogopwa.

5 Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea,

katika neno lake naweka tumaini langu.

6 Nafsi yangu inamngojea Bwana

kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,

naam, kuliko walinzi

waingojeavyo asubuhi.

7 Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu,

maana kwa Mwenyezi Mungu kuna upendo usiokoma,

na kwake kuna ukombozi kamili.

8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli

kutoka dhambi zao zote.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também