Publicidade

Salmos 138

Maombi ya shukrani
Zaburi ya Daudi.

1 Nitakusifu wewe, Ee Mwenyezi Mungu, kwa moyo wangu wote,

mbele ya "miungu" nitaimba sifa zako.

2 Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu,

nami nitalisifu jina lako

kwa ajili ya upendo wako

na uaminifu,

kwa maana umeitukuza ahadi yako

zaidi ya jina lako.

3 Nilipoita, ulinijibu;

ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.

4 Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Mwenyezi Mungu,

wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako.

5 Wao na waimbe kuhusu njia za Mwenyezi Mungu,

kwa maana utukufu wa Mwenyezi Mungu ni mkuu.

6 Ingawa Mwenyezi Mungu yuko juu,

humwangalia mnyonge,

bali mwenye kiburi

yeye anamjua kutokea mbali.

7 Nijapopita katikati ya shida,

wewe unayahifadhi maisha yangu,

unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu,

kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.

8 Mwenyezi Mungu atatimiza kusudi lake kwangu,

Ee Mwenyezi Mungu, upendo wako wadumu milele:

usiziache kazi za mikono yako.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-