Publicidade

Salmos 127

Bila Mwenyezi Mungu, kazi ya mwanadamu haifai
Wimbo wa kwenda juu. Wa Sulemani.

1 Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba,

wajengao hufanya kazi bure.

Mwenyezi Mungu asipoulinda mji,

walinzi wakesha bure.

2 Mnajisumbua bure kuamka mapema

na kuchelewa kulala,

mkitaabikia chakula:

kwa maana yeye huwapa usingizi wapendwa wake.

3 Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu,

uzao ni zawadi kutoka kwake.

4 Kama mishale mikononi mwa shujaa

ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

5 Heri mtu ambaye podo lake

limejazwa nao.

Hawataaibishwa wanaposhindana

na adui zao langoni.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-18_06-35-37-