Publicidade

Vida

Por Bíblia Online

A vida é um dom precioso de Deus. Desde a concepção até a eternidade, as Escrituras revelam o propósito, o valor e a plenitude da vida que o Senhor nos oferece.

Deus, o autor da vida

O Senhor é quem dá a vida e a sustenta. Cada ser humano foi formado por suas mãos com propósito e intenção divina.

Bwana Mwenyezi Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

kazi zako ni za ajabu,

ninajua hayo kikamilifu.

Umbile langu halikufichika kwako,

nilipoumbwa mahali pa siri.

Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

Siku zangu zote ulizonipangia

ziliandikwa katika kitabu chako

kabla haijakuwa hata moja.

Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,

katika nuru yako twaona nuru.

Nitamwimbia Mwenyezi Mungu maisha yangu yote;

nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.

A vida em Cristo

Jesus é o caminho, a verdade e a vida. Nele encontramos sentido, plenitude e a promessa de vida abundante e eterna.

Isa akawaambia, "Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.

Mwizi huja ili aibe, aue na aangamize. Mimi nimekuja ili wapate uzima, kisha wawe nao tele.

Isa akamwambia, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi; na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?"

Isa akawaambia, "Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe.

Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yanavyosema, vijito vya maji ya uzima vitatiririka kutoka ndani yake."

Nimesulubiwa pamoja na Al-Masihi, wala si mimi tena ninayeishi, bali Al-Masihi ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili., aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

Nimesulubiwa pamoja na Al-Masihi, wala si mimi tena ninayeishi, bali Al-Masihi ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili., aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

Vivendo com sabedoria

A Bíblia nos orienta a viver com sabedoria, aproveitando bem o tempo, guardando o coração e buscando a vontade de Deus para cada dia.

Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,

ili tujipatie moyo wa hekima.

Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia,

nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.

Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,

maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,

maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,

yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.

Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake,

bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia.

Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima,

lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.

Kumcha Mwenyezi Mungu ni chemchemi ya uzima,

ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.

Yeye afuatiaye haki na upendo

hupata uzima, mafanikio na heshima.

Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu.

A vida no dia a dia

Cada dia é uma oportunidade de glorificar a Deus. A Escritura nos chama a viver com propósito, confiança e fé prática.

Nioneshe njia zako, Ee Mwenyezi Mungu,

nifundishe mapito yako,

Hakika wema na upendo vitanifuata

siku zote za maisha yangu,

nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu

milele.

Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,

bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu

na fungu langu milele.

Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.

Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,

uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.

Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu

na kumtafuta hekaluni mwake.

Tulia mbele za Mwenyezi Mungu

na umngojee kwa uvumilivu;

usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,

wanapotekeleza mipango yao miovu.

Sitasahau mausia yako kamwe,

kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.

Prioridades e eternidade

Jesus nos lembra que a vida é mais que comida e o corpo mais que roupa. O que importa é buscar o Reino de Deus e viver para a eternidade.

Msiwe na wasiwasi

"Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao ndege? Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake?

Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake?

Ndipo akawaita umati ule wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, "Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu."

Ndipo Isa akawaambia, "Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo."

Nao uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma.

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Al-Masihi Isa Bwana wetu.

Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake.

Kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.

Onyo dhidi ya kuikataa neema ya Mwenyezi Mungu

Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao hakuna mtu atakayemwona Bwana.

Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza, ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote.

Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote kama watu wanaomtumikia Bwana Isa, na si wanadamu, kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Isa Al-Masihi mnayemtumikia.

Kujaribiwa

Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji lile la uzima Mungu alilowaahidia wale wanaompenda.

Aina mbili za hekima

Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aioneshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.

Kwa maana,

"Yeyote apendaye uzima

na kuona siku njema,

basi auzuie ulimi wake usinene mabaya,

na midomo yake isiseme hila.

Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema;

lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

Kila chenye pumzi na kimsifu Mwenyezi Mungu.

Msifuni Mwenyezi Mungu!

Kila jambo lina wakati wake

Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo,

nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu:

Ninakuamuru leo kwamba umpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.

Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Mwenyezi Mungu, Mungu wako.

Siku zetu za kuishi ni miaka sabini,

au miaka themanini ikiwa tuna nguvu,

lakini yote ni ya shida na taabu,

nazo zapita haraka, nasi twatoweka.

"Ee Mwenyezi Mungu, nijulishe mwisho wa maisha yangu

na hesabu ya siku zangu;

nijalie kujua jinsi maisha yangu

yanavyopita upesi.

Umefanya maisha yangu mafupi kama nyanda;

muda wangu wa kuishi ni kama

hauna thamani kwako.

Maisha ya kila mwanadamu

ni kama pumzi.

Hakika kila binadamu ni kama njozi

aendapo huku na huko:

hujishughulisha na mengi, lakini ni ubatili;

anakusanya mali nyingi,

wala hajui ni nani atakayejifaidi nayo.

Yeyote kati yenu anayependa uzima

na kutamani kuziona siku nyingi njema,

basi auzuie ulimi wake na mabaya,

na midomo yake kutokana na kusema uongo.

Aache uovu, atende mema,

aitafute amani na kuifuatilia.

Mvi ni taji la utukufu;

hupatikana kwa maisha ya uadilifu.

Kama uso uonekanavyo kwenye maji,

ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonesha alivyo.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-28_14-13-17-