Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wafalme 6:1-3,19,20

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Solomoni Ajenga Hekalu

1 Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Bwana.

2 Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili ya Bwana lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini,6:2 Dhiraa 60 ni sawa na mita 27. upana wa dhiraa ishirini6:2 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. na kimo cha dhiraa thelathini6:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. kwenda juu. 3 Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu.

19 Ndani ya Hekalu akatengeneza sehemu takatifu ya ndani, kwa ajili ya kuweka Sanduku la Agano la Bwana. 20 Sehemu takatifu ya ndani ilikuwa na upana, urefu na kimo cha dhiraa ishirini ndani kwa ndani. Akaifunika ndani kwa dhahabu safi, pia akaifunika madhabahu ya mierezi vivyo hivyo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani katika Israeli, katika mwezi wa Zivu6:1 mwezi wa tano katika kalenda ya Kiyahudi, uliokuwa mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu.

    2 Hekalu ambalo Mfalme Sulemani alilijenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini6:2 Dhiraa 60 ni sawa na mita 27., upana wa dhiraa ishirini6:2 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9., na kimo cha dhiraa thelathini6:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. kwenda juu. 3 Baraza iliyokuwa mbele ya ukumbi mkuu wa Hekalu iliongeza upana wa Hekalu kwa dhiraa ishirini, na kuchomoza dhiraa kumi mbele ya Hekalu.

    19 Ndani ya Hekalu akatengeneza mahali patakatifu pa kuliweka Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu. 20 Mahali patakatifu palikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, upana wa dhiraa ishirini, na kimo cha dhiraa ishirini. Akapafunika upande wa ndani, na madhabahu ya mwerezi pia, kwa dhahabu safi.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya wana wa Israeli kutoka nchini Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu,6:1 Zivu ni mwezi wa pili katika kalenda ya Israeli. ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya BWANA. 2 Eze 41:1Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea BWANA, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini. 3 Na ukumbi mbele ya hekalu la nyumba, urefu wake ulikuwa mikono ishirini, kadiri ya upana wa nyumba; na upana wake mikono kumi mbele ya nyumba.

    19 Kut 40:20;1 Fal 8:6-10Akaweka tayari chumba cha ndani katikati ya nyumba ndani, ili atie humo sanduku la Agano la BWANA. 20 Na ndani yake chumba hicho cha ndani mlikuwa na nafasi, mikono ishirini urefu, na mikono ishirini upana, na mikono ishirini kwenda juu kwake; akaifunika na dhahabu safi. Akaifunika madhabahu nayo kwa mwerezi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.