Sulemani ajenga Hekalu
1 Katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani katika Israeli, katika mwezi wa Zivu6:1 mwezi wa tano katika kalenda ya Kiyahudi, uliokuwa mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu.
2 Hekalu ambalo Mfalme Sulemani alilijenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini6:2 Dhiraa 60 ni sawa na mita 27., upana wa dhiraa ishirini6:2 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9., na kimo cha dhiraa thelathini6:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. kwenda juu. 3 Baraza iliyokuwa mbele ya ukumbi mkuu wa Hekalu iliongeza upana wa Hekalu kwa dhiraa ishirini, na kuchomoza dhiraa kumi mbele ya Hekalu.
19 Ndani ya Hekalu akatengeneza mahali patakatifu pa kuliweka Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu. 20 Mahali patakatifu palikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, upana wa dhiraa ishirini, na kimo cha dhiraa ishirini. Akapafunika upande wa ndani, na madhabahu ya mwerezi pia, kwa dhahabu safi.