Sulemani ajenga hekalu
1 Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya wana wa Israeli kutoka nchini Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu,6:1 Zivu ni mwezi wa pili katika kalenda ya Israeli. ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya BWANA. 2 Eze 41:1Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea BWANA, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini. 3 Na ukumbi mbele ya hekalu la nyumba, urefu wake ulikuwa mikono ishirini, kadiri ya upana wa nyumba; na upana wake mikono kumi mbele ya nyumba.
19 Kut 40:20;1 Fal 8:6-10Akaweka tayari chumba cha ndani katikati ya nyumba ndani, ili atie humo sanduku la Agano la BWANA. 20 Na ndani yake chumba hicho cha ndani mlikuwa na nafasi, mikono ishirini urefu, na mikono ishirini upana, na mikono ishirini kwenda juu kwake; akaifunika na dhahabu safi. Akaifunika madhabahu nayo kwa mwerezi.