Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 15:3,9,13,15,22,23

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

3 Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ngʼombe na kondoo, ngamia na punda.’ "

9 Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ngʼombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.

13 Samweli alipomfikia, Sauli akamwambia, "Bwana akubariki! Nimetimiza yale Bwana aliniagiza."

15 Sauli akajibu, "Askari wamewaleta kutoka kwa Waamaleki, waliwaacha wale kondoo na ngʼombe wazuri ili kuwatoa dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, lakini tuliwaangamiza kabisa wengine wote."

22 Lakini Samweli akajibu:

"Je, Bwana anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu

kama vile kuitii sauti ya Bwana?

Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu,

nako kusikia ni bora

kuliko mafuta ya kondoo dume.

23 Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,

nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.

Kwa sababu umelikataa neno la Bwana,

naye amekukataa wewe

kuendelea kuwa mfalme."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    3 Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wale wanaonyonya, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.’ "

    9 Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi, na kondoo na ng’ombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona, na kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.

    13 Samweli alipomfikia, Sauli akamwambia, "Mwenyezi Mungu akubariki! Nimetimiza yale Mwenyezi Mungu aliyoniagiza."

    15 Sauli akajibu, "Askari wamewaleta kutoka kwa Waamaleki, waliwaacha wale kondoo na ng’ombe wazuri ili kuwatoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, lakini tuliwaangamiza kabisa wengine wote."

    22 Lakini Samweli akajibu:

    "Je, Mwenyezi Mungu anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu

    kama vile kuitii sauti ya Mwenyezi Mungu?

    Kutii ni bora kuliko dhabihu,

    nako kusikia ni bora

    kuliko mafuta ya kondoo dume.

    23 Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,

    nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.

    Kwa sababu umelikataa neno la Mwenyezi Mungu,

    naye amekukataa wewe

    kuendelea kuwa mfalme."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    3 Law 27:28;Yos 6:17;Kut 20:5;Isa 14:21;Mwa 3:17;Yos 7:24Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda. 9 Mit 15:27;1 Tim 6:10Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.

    13 Mwa 14:19;Amu 17:2;Rut 3:2;Lk 18:11Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA. 15 Mwa 3:12;Mit 28:13Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng’ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.

    22 Zab 50:8,9;Mit 21:3;Isa 1:11;Yer 7:22;Amo 5:21,24;Mik 6:6;Mt 9:13;12:7;Ebr 10:6;Kut 19:5;Mhu 5:1;Yer 7:23;Hos 6:6;Mt 5:24;9:13;Mk 12:33Naye Samweli akasema,

    Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu

    Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?

    Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,

    Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.

    23 Kum 18:10Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,

    Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago;

    Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA,

    Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.