3 Law 27:28;Yos 6:17;Kut 20:5;Isa 14:21;Mwa 3:17;Yos 7:24Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda. 9 Mit 15:27;1 Tim 6:10Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.
13 Mwa 14:19;Amu 17:2;Rut 3:2;Lk 18:11Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA. 15 Mwa 3:12;Mit 28:13Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng’ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.
22 Zab 50:8,9;Mit 21:3;Isa 1:11;Yer 7:22;Amo 5:21,24;Mik 6:6;Mt 9:13;12:7;Ebr 10:6;Kut 19:5;Mhu 5:1;Yer 7:23;Hos 6:6;Mt 5:24;9:13;Mk 12:33Naye Samweli akasema,
Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.
23 Kum 18:10Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,
Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago;
Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA,
Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.