3 Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wale wanaonyonya, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.’ "
9 Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi, na kondoo na ng’ombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona, na kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.
13 Samweli alipomfikia, Sauli akamwambia, "Mwenyezi Mungu akubariki! Nimetimiza yale Mwenyezi Mungu aliyoniagiza."
15 Sauli akajibu, "Askari wamewaleta kutoka kwa Waamaleki, waliwaacha wale kondoo na ng’ombe wazuri ili kuwatoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, lakini tuliwaangamiza kabisa wengine wote."
22 Lakini Samweli akajibu:
"Je, Mwenyezi Mungu anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu
kama vile kuitii sauti ya Mwenyezi Mungu?
Kutii ni bora kuliko dhabihu,
nako kusikia ni bora
kuliko mafuta ya kondoo dume.
23 Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,
nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.
Kwa sababu umelikataa neno la Mwenyezi Mungu,
naye amekukataa wewe
kuendelea kuwa mfalme."