Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 21:1-6

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Daudi Huko Nobu

1 Daudi akaenda Nobu, kwa Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akatetemeka alipokutana naye, akamuuliza, "Kwa nini uko peke yako? Kwa nini hukufuatana na mtu yeyote?"

2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, "Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu yeyote asijue chochote kuhusu kazi yako wala maagizo yako!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia tukutane mahali fulani. 3 Sasa basi, una nini mkononi? Nipatie mikate mitano au chochote unachoweza kupata."

4 Lakini kuhani akamjibu Daudi, "Sina mkate wowote wa kawaida kwa sasa. Hata hivyo, ipo hapa mikate iliyowekwa wakfu, iwapo watu wamejitenga na wanawake."

5 Daudi akajibu, "Hakika tumejitenga na wanawake kwa siku hizi chache kama kawaida ya ninapotoka kwenda kwenye shughuli. Navyo vyombo vya wale vijana huwa ni vitakatifu hata kwenye safari ya kawaida, si zaidi sana leo vyombo vyao vitakuwa ni vitakatifu?" 6 Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwepo mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonyesho iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za Bwana na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Daudi akaenda Nobu, kwa Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akatetemeka alipokutana naye, akamuuliza, "Kwa nini uko peke yako? Kwa nini hukufuatana na mtu yeyote?"

    2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, "Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu yeyote asijue chochote kuhusu kazi niliyokutuma kuifanya, wala maagizo niliyokupa!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia mahali pa kukutana. 3 Sasa basi, una nini mkononi? Nipatie mikate mitano au chochote unachoweza kupata."

    4 Lakini kuhani akamjibu Daudi, "Sina mkate wowote wa kawaida kwa sasa. Hata hivyo, ipo hapa mikate iliyowekwa wakfu, iwapo watu wamejitenga na wanawake."

    5 Daudi akajibu, "Hakika tumejitenga na wanawake kwa siku hizi chache kama kawaida ya ninapotoka kwenda kwenye shughuli. Navyo vyombo vya wale vijana huwa ni vitakatifu hata kwenye safari ya kawaida, si zaidi sana leo vyombo vyao vitakuwa ni vitakatifu?" 6 Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwa na mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonesho, iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za Mwenyezi Mungu na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mt 12:3-4;Mk 2:25-26;Lk 6:3;1 Sam 22:19;Neh 11:32;Isa 10:32;1 Sam 14:3Basi Daudi akaenda Nobu kwa Ahimeleki, kuhani. Ahimeleki akaenda kumlaki Daudi, akitetemeka, akamwambia, Kwa nini uko peke yako, wala hapana mtu pamoja nawe? 2 Mwa 27:20-24;1 Sam 19:11;22:22;1 Fal 13:18;Zab 119:29;141:3;Mit 29:25;Gal 2:12,13;Kol 3:9Daudi akamwambia Ahimeleki, kuhani, Mfalme ameniagiza shughuli, akaniambia, Asijue mtu awaye yote habari ya shughuli hii ninayokutuma, wala ya neno hili ninalokuamuru; nami nimewaagiza vijana waende mahali fulani. 3 Kuna nini basi, chini ya mkono wako? Nipe mkononi mwangu mikate mitano, au chochote ulicho nacho hapa. 4 Kut 25:30;Law 24:5;Mt 12:4;Kut 19:15;Zek 7:3Yule kuhani akamjibu Daudi, akasema, Hapana mikate ya kawaida chini ya mkono wangu, ila mikate mitakatifu; ikiwa wale vijana wamejitenga na wanawake. 5 1 The 4:4;Law 8:26Naye Daudi akamjibu kuhani, akamwambia, Hakika tumejitenga na wanawake siku hizi tatu; napo nilipotoka, vyombo vya vijana hawa vilikuwa vitakatifu, ingawa ilikuwa safari ya kawaida; basi leo je! Vyombo vyetu havitakuwa vitakatifu zaidi? 6 Law 24:5-9;Mt 12:3;Mk 2:25;Lk 6:3Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za BWANA, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.