Daudi huko Nobu
1 Daudi akaenda Nobu, kwa Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akatetemeka alipokutana naye, akamuuliza, "Kwa nini uko peke yako? Kwa nini hukufuatana na mtu yeyote?"
2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, "Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu yeyote asijue chochote kuhusu kazi niliyokutuma kuifanya, wala maagizo niliyokupa!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia mahali pa kukutana. 3 Sasa basi, una nini mkononi? Nipatie mikate mitano au chochote unachoweza kupata."
4 Lakini kuhani akamjibu Daudi, "Sina mkate wowote wa kawaida kwa sasa. Hata hivyo, ipo hapa mikate iliyowekwa wakfu, iwapo watu wamejitenga na wanawake."
5 Daudi akajibu, "Hakika tumejitenga na wanawake kwa siku hizi chache kama kawaida ya ninapotoka kwenda kwenye shughuli. Navyo vyombo vya wale vijana huwa ni vitakatifu hata kwenye safari ya kawaida, si zaidi sana leo vyombo vyao vitakuwa ni vitakatifu?" 6 Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwa na mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonesho, iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za Mwenyezi Mungu na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.