Daudi na Mkate Mtakatifu
1 Mt 12:3-4;Mk 2:25-26;Lk 6:3;1 Sam 22:19;Neh 11:32;Isa 10:32;1 Sam 14:3Basi Daudi akaenda Nobu kwa Ahimeleki, kuhani. Ahimeleki akaenda kumlaki Daudi, akitetemeka, akamwambia, Kwa nini uko peke yako, wala hapana mtu pamoja nawe? 2 Mwa 27:20-24;1 Sam 19:11;22:22;1 Fal 13:18;Zab 119:29;141:3;Mit 29:25;Gal 2:12,13;Kol 3:9Daudi akamwambia Ahimeleki, kuhani, Mfalme ameniagiza shughuli, akaniambia, Asijue mtu awaye yote habari ya shughuli hii ninayokutuma, wala ya neno hili ninalokuamuru; nami nimewaagiza vijana waende mahali fulani. 3 Kuna nini basi, chini ya mkono wako? Nipe mkononi mwangu mikate mitano, au chochote ulicho nacho hapa. 4 Kut 25:30;Law 24:5;Mt 12:4;Kut 19:15;Zek 7:3Yule kuhani akamjibu Daudi, akasema, Hapana mikate ya kawaida chini ya mkono wangu, ila mikate mitakatifu; ikiwa wale vijana wamejitenga na wanawake. 5 1 The 4:4;Law 8:26Naye Daudi akamjibu kuhani, akamwambia, Hakika tumejitenga na wanawake siku hizi tatu; napo nilipotoka, vyombo vya vijana hawa vilikuwa vitakatifu, ingawa ilikuwa safari ya kawaida; basi leo je! Vyombo vyetu havitakuwa vitakatifu zaidi? 6 Law 24:5-9;Mt 12:3;Mk 2:25;Lk 6:3Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za BWANA, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa.