7 Ndipo Nathani akamwambia Daudi, "Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli. 9 Kwa nini ulilidharau neno la Bwana kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria, Mhiti kwa upanga na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni.
13 Ndipo Daudi akamjibu Nathani, "Nimefanya dhambi dhidi ya Bwana."
Nathani akamjibu, "Bwana amekuondolea dhambi yako. Hutakufa.