7 Ndipo Nathani akamwambia Daudi, "Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli. 9 Kwa nini ulilidharau neno la Mwenyezi Mungu kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria Mhiti kwa upanga, na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni.
13 Ndipo Daudi akamjibu Nathani, "Nimefanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu."
Nathani akamjibu, "Mwenyezi Mungu amekuondolea dhambi yako. Hutakufa.