7 1 Sam 16:13;2 Sam 7:8Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nilikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa kutoka kwa mkono wa Sauli; 9 Mwa 9:5,6;1 Sam 15:19;Law 26:15,16;Hes 15:31;Mit 13:13;Isa 5:24;2 Sam 11:15Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa Waamoni. 13 1 Sam 15:24;2 Sam 24:10;Ayu 7:20;Zab 32:5;51:4;Mit 28:13;Zab 32:1;Mik 7:18;Zek 3:4Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.
2 Samweli 12:7,9,13
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
7 Ndipo Nathani akamwambia Daudi, "Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli. 9 Kwa nini ulilidharau neno la Mwenyezi Mungu kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria Mhiti kwa upanga, na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni.
13 Ndipo Daudi akamjibu Nathani, "Nimefanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu."
Nathani akamjibu, "Mwenyezi Mungu amekuondolea dhambi yako. Hutakufa.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
7 Ndipo Nathani akamwambia Daudi, "Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli. 9 Kwa nini ulilidharau neno la Bwana kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria, Mhiti kwa upanga na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni.
13 Ndipo Daudi akamjibu Nathani, "Nimefanya dhambi dhidi ya Bwana."
Nathani akamjibu, "Bwana amekuondolea dhambi yako. Hutakufa.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.