2 Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema:
"Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu!
Umekuwa makao ya mashetani
na makazi ya kila pepo mchafu,
makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.
3 Kwa maana mataifa yote yamekunywa
mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.
Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi nao,
nao wafanyabiashara wa dunia
wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake."
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema:
"Tokeni katikati yake, enyi watu wangu,
ili msije mkashiriki dhambi zake,
ili msije mkapatwa na pigo lake lolote;