14 Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanyabiashara wa nguo za zambarau, mwenyeji wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Bwana akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo. 15 Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumba yake, alitukaribisha nyumbani kwake akisema, "Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana, karibuni mkae nyumbani mwangu." Naye akatushawishi.
30 Kisha akawaleta nje akisema, "Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?"
31 Wakamjibu, "Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako." 32 Wakamwambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwako nyumbani mwake. 33 Wakati ule ule, yule mkuu wa gereza akawachukua, akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa.