14 Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanyabiashara wa nguo za zambarau, raia wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Mwenyezi Mungu akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo. 15 Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumba yake, alitukaribisha nyumbani mwake, akisema, "Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana Isa, karibuni mkae nyumbani mwangu." Naye akatushawishi.
30 Kisha akawaleta nje akisema, "Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?"
31 Wakamjibu, "Mwamini Bwana Isa Al-Masihi, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako." 32 Wakamwambia neno la Bwana Isa, yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake. 33 Wakati ule ule, yule mkuu wa gereza akawachukua, akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa.