14 Yn 6:44Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo. 15 Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatusihi sana.
30 Mdo 2:37kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. 32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. 33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.