Pular para o conteúdo
Publicidade

Danieli 2:17,18,20-23

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

17 Ndipo Danieli akarudi nyumbani kwake na kuwaeleza rafiki zake Hanania, Mishaeli na Azaria jambo hilo. 18 Aliwasihi waombe rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hii, ili yeye na rafiki zake wasije wakauawa pamoja na wenye hekima wengine wa Babeli. 20 na akasema:

"Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele;

hekima na uweza ni vyake.

21 Yeye hubadili nyakati na majira;

huwaweka wafalme na kuwaondoa.

Huwapa hekima wenye hekima,

na maarifa wenye ufahamu.

22 Hufunua siri na mambo yaliyofichika;

anajua yale yaliyo gizani,

nayo nuru hukaa kwake.

23 Ninakushukuru na kukuhimidi,

Ee Mungu wa baba zangu:

Umenipa hekima na uwezo,

umenijulisha kile tulichokuomba,

umetujulisha ndoto ya mfalme."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    17 Ndipo Danieli akarudi nyumbani mwake na kuwaeleza rafiki zake Hanania, Mishaeli na Azaria jambo hilo. 18 Aliwasihi waombe rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hii, ili yeye na rafiki zake wasije wakauawa pamoja na wenye hekima wengine wa Babeli. 20 akasema:

    "Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele;

    hekima na uweza ni vyake.

    21 Yeye hubadili nyakati na majira;

    huwaweka wafalme na kuwaondoa.

    Huwapa hekima wenye hekima,

    na maarifa wenye ufahamu.

    22 Hufunua siri na mambo yaliyofichika;

    anajua yale yaliyo gizani,

    nayo nuru hukaa kwake.

    23 Ninakushukuru na kukuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu:

    Umenipa hekima na uwezo;

    umenijulisha kile tulichokuomba,

    umetujulisha ndoto ya mfalme."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    17 Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; 18 ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. 20 Zab 113:2;147:5;Ayu 12:13;Yer 32:19;Mt 6:13Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. 21 1 Nya 29:30;Est 1:13;Dan 7:25;4:17;Ayu 12:18;Zab 75:6,7;Yer 27:5;Yak 1:5Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; 22 Ayu 12:22;Ebr 4:13;Zab 25:14;139:11,12;Dan 5:11yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake. 23 Amo 3:7Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.