Mungu afumbua ndoto ya mfalme Nebukadneza
17 Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; 18 ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. 20 Zab 113:2;147:5;Ayu 12:13;Yer 32:19;Mt 6:13Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. 21 1 Nya 29:30;Est 1:13;Dan 7:25;4:17;Ayu 12:18;Zab 75:6,7;Yer 27:5;Yak 1:5Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; 22 Ayu 12:22;Ebr 4:13;Zab 25:14;139:11,12;Dan 5:11yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake. 23 Amo 3:7Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme.