17 Ndipo Danieli akarudi nyumbani mwake na kuwaeleza rafiki zake Hanania, Mishaeli na Azaria jambo hilo. 18 Aliwasihi waombe rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hii, ili yeye na rafiki zake wasije wakauawa pamoja na wenye hekima wengine wa Babeli. 20 akasema:
"Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele;
hekima na uweza ni vyake.
21 Yeye hubadili nyakati na majira;
huwaweka wafalme na kuwaondoa.
Huwapa hekima wenye hekima,
na maarifa wenye ufahamu.
22 Hufunua siri na mambo yaliyofichika;
anajua yale yaliyo gizani,
nayo nuru hukaa kwake.
23 Ninakushukuru na kukuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu:
Umenipa hekima na uwezo;
umenijulisha kile tulichokuomba,
umetujulisha ndoto ya mfalme."