6 Bwana Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi.
Uzima Na Mauti
11 Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza. 12 Hakiko juu mbinguni, ili uulize, "Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?" 13 Wala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, "Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?" 14 La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.