6 Kum 10:16;Eze 11:19BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.
Ushawishi wa kuchagua uhai
11 Isa 45:19Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali. 12 Rum 10:6-8;Mit 30:4;Yn 3:13Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya? 13 Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya? 14 Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.