Pular para o conteúdo
Publicidade

Kumbukumbu la Torati 19

Sheria kuhusu miji ya ukimbizi

1 Yos 20:1-9 BWANA, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa yenye nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nawe ukawafuata, na kukaa katika miji yao, na katika nyumba zao; 2 Yos 20:2 itenge miji mitatu iwe kwako katikati ya nchi yako, akupayo BWANA, Mungu wako, kuimiliki. 3 Itengeze njia, igawanye na mipaka ya nchi yako, akurithishayo BWANA, Mungu wako, iwe mafungu matatu, ili kwamba kila mwenye kuua mtu apate kukimbilia huko. 4 Na hii ndiyo hukumu ya mwenye kuua mtu, atakayekimbilia huko awe hai; atakayemwua mwenziwe pasipo kukusudia, wala hakumchukia tangu hapo; 5 kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai; 6 asije akaandamiwa mwuaji na mwenye kulipiza kisasi cha damu, moyo wake ukali na hasira, akampata kwa njia kuwa ndefu, akamwua; wala hana haki ya kuuawa, kwa kuwa hakumchukia tangu hapo. 7 Kwa sababu hii ninakuamuru, na kukuambia, Ujitengee miji mitatu. 8 Mwa 15:18 Na kama BWANA, Mungu wako, akiueneza mpaka wako kama alivyowaapia baba zako, akakupa na nchi yote aliyoahidi kwamba atawapa baba zako; 9 Yos 20:7 nawe ukiyashika maagizo haya yote nikuagizayo leo, na kuyafanya, kumpenda BWANA, Mungu wako, na kwenda sikuzote katika njia zake, ndipo ujiongezee miji mitatu tena, pamoja na mitatu ile; 10 isije ikamwagika damu ya asiye makosa kati ya nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi, ikawa na damu juu yako. 11 Kut 21:12;Hes 35:16;Mit 28:17;29:10;1 Yoh 3:15 Lakini mtu awaye yote akimchukia mwenziwe na kumwotea na kumwinukia, akampiga hata akafa; naye akakimbilia miji hii mmojawapo; 12 ndipo wazee wa mji wake wapeleke ujumbe kumtwaa huko, na kumwua katika mkono wa mwenye kulipiza kisasi cha damu, apate kufa. 13 1 Fal 2:31 Jicho lako lisimhurumie, lakini uondoe damu ya asiye makosa katika Israeli, ili upate kufanikiwa.

Mipaka ya ardhi

14 Kum 27:17;Ayu 24:2;Mit 22:28;Hos 5:10 Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.

Sheria kuhusu mashahidi

15 Hes 35:30;Kum 17:6;Mt 18:16;Yn 8:17;19:31;2 Kor 13:1;1 Tim 5:19;Ebr 10:28 Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wowote, wala kwa dhambi yoyote, katika makosa akosayo yoyote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu. 16 Zab 27:12;1 Fal 21:13 Shahidi mdhalimu akimwinukia mtu yeyote na kushuhudia juu yake ya upotoe; 17 ndipo wale watu washindanao kwa mambo yale na wasimame wote wawili mbele za BWANA, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo; 18 nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye; 19 Mit 19:5;Dan 6:24 ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. 20 Kum 17:13;21:21 Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. 21 Kut 21:23-25;Law 24:19-20;Mt 5:38 Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também