Ishara Za Mose
1 Mose akamjibu, "Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwana hakukutokea’?"
2 Ndipo Bwana akamwambia, "Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?"
Akajibu, "Fimbo."
3 Bwana akasema, "Itupe chini."
Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4 Kisha Bwana akamwambia, "Nyoosha mkono wako umkamate mkiani." Basi Mose akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 5 Bwana akasema, "Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Bwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe."