Ishara za Musa
1 Musa akamjibu, "Itakuwaje wasiponiamini au kunisikiliza, waseme, ‘Mwenyezi Mungu hakukutokea’?"
2 Ndipo Mwenyezi Mungu akamuuliza, "Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?"
Akamjibu, "Ni fimbo."
3 Mwenyezi Mungu akasema, "Itupe chini."
Musa akaitupa fimbo chini, nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia, "Nyoosha mkono wako umkamate kwenye mkia." Basi Musa akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 5 Mwenyezi Mungu akasema, "Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe."